Tag Archives: The Will of Heaven

Mapenzi ya Mbinguni

Watu wengi duniani wanasubiri mwokozi wao, Maitreya wao au Imam wao arudi. Lakini Mungu ametuma Ujumbe Mpya duniani, Ujumbe wa kuandaa ubinadamu kwa mabadiliko makubwa ambayo yatatokea na kwa mawasiliano na ulimwengu wa waangavu, Mawasiliano ambayo yatakuwa ya hatari zaidi kuliko vile watu wengi wanatambua.

 

Kiroho cha binadamu kinamomonyoka duniani, asili ya kweli ya kiroho cha binadamu. Asili ya ndani ya kila mtu polepole inaanza kuwa baidi jamii yenyu ikizidi kuwa ya kiteknolojia na ya kidunia. Mgawanyiko kati ya dini ni kubwa sana na ya kuharibu, hata mgawanyiko ndani ya dini, yataongeza kwa migogoro na mateso ya binadamu katika siku zijazo, kama vile zivyo sasa.

 

Ukiangalia dunia kwa uaminifu ni utatambua kwamba matatizo yake yamezidi kushinda uwezo wa binadamu na uelewa wake. Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko yanayokuja duniani yanazidi yale watu binafsi na taasisi zinaweza kufahamu na kujadiliana nazo.

 

Ubinadamu umefikia katika kizingiti kikubwa cha mageuko. Hauwezi kurudi katika hali yake ya zamani. Hauwezi kurudi nyuma katika historia yake. Na hauwezi tu kuthibitisha imani zilizogawanywa na zina matata katika mila zake za kidini, ambazo zilianzishwa na Mungu.

 

Ufunuo wa Mungu lazima sasa uje tena na umekuja tena, na Mtume ametumwa duniani – mtu mnyenyekevu, mtu asiye na cheo kikubwa katika kijamii, mtu asiye na madai makubwa za kibinafsi na mafanikio, mtu ambaye maisha yake imehifadhiwa na kuelekezwa kwa dhamira hii peke yake.

 

Watu watabishana kuhusu haya, bila shaka, hawatataka au hawataweza kufikiria upya msimamo wao na kuwa wazi kwa Ufunuo Mpya. Wanafikiri kuwa wanaelewa mapenzi ya Mungu na dhamira yake kwa watu wa dunia hii. Wanafikiri wanaelewa maana ya Ufunuo na wakati unaweza kutokea.

 

Wanafikiri wanaelewa. Lakini ni nani anaweza kuyaelewa haya kikamilifu? Nani mwenye hekima na upana na uwezo wa kuyaelewa haya kikamilifu? Hakika haya lazima yazidi ufahamu wa mwanadamu. Na hakika lazima kuwe na unyenyekevu na uaminifu wa kutosha wa kutambua kwamba watu hawawezi kutabiri wakati na jinsi Muumba wa Ulimwengu wote atazungumza katika sayari hii moja ndogo.

 

Ujinga na kiburi cha binadamu unaungana hapa na kufomu mchanganyiko wa hatari, mchanganyiko wa ukali na ukandamizaji. Wa uchovu na kirahi. Wa upendeleo na utaoendelea kugawanya familia ya binadamu, mgawanyiko ambao unaweza kuwadhoofisha mkikabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo yanakuja duniani.

 

Ujumbe Mpya uko hapa katika fomu safi, na kwa mara ya kwanza mutakuwua na uwezo wa kusikia Sauti ya Ufunuo. Ilikuwa ni sauti kama hii iliyonena na Musa na Yesu, Buddha na Muhammad na Walimu wengine wakuu ambao hawajulikani katika mwenendo wa historia ya binadamu.

 

Hakuna wakati wa makosa sasa. Hatari ni kubwa mno. Kila kitu kinachofanywa na Ufunuo Mpya kinafanywa ndio uwe wazi kabisa. Unatoa Ufafanuzi wake mwenyewe, Mafundisho yake yenyewe, kwa kuwa haya hayawezi kuachwa kwa utafsiri wa binadamu.

 

Hamuna wakati wa kutosha na ubinadamu haujajiandaa ndio uweze kukabiliana na dunia mpya ya rasilimali zinazopungka, kwa kukabiliana na hali halisi na matatizo ya kuibuka ndani ya Jumuiya Kubwa ya maisha ulimwenguni.

 

Muko katika kizingiti kikubwa, na kwako wewe kama mtu binafsii ina maanisha kuwa maisha yako inaharakishwa kukabiliana na kizingiti hiki, kujiandaa ili uweze kukabiliana na kizingiti hiki, na kushirikiana na kizingiti hiki.

 

Lakini hii inawezekanaje bila Ufunuo Mpya kutoka kwa Mungu? Hakuna mtu duniani aliye na hekima, uwezo na uelewa wa kuyatatua yale yote binadamu atakabiliana nayo akipita katika kizingiti hiki na kuingia katika dunia mpya na ya changamoto.

 

Ni nani duniani anayeweza kutayarisha binadamu ili aweze kukabiliana na ulemwengu, Ushiriki mkubwa, ushiriki ambao hata saa hizi unatokea, kwa siri, unafanywa na vikundi ambavyo viko hapa kupata faida kupitia ujinga na ushirikina wa binadamu?

 

Kama wewe kwa kweli ni mwaminifu, lazima ugundue kuwa hakuna aliye na upana wa uelewa huu, uwezo huu. Hakuna yeyote duniani anayeelewa Jumuia Kubwa ya maisha. Na kile watu wanafikiri ni makadirio ya hofu zao, fantasies zao, na haya yote hayatoi picha sahihi kuhusu yale ambayo mtakabiliwa nayo.

 

Asili ya kweli ya kiroho cha binadamu sasa imefumbwa, imepotoshwa, imeshikiliwa na mila na desturi na tafsiri kwa kiasi kikubwa hadi mila kuu ya dunia, ambayo inaweza kutoa hatua zile lazima muchukue, zinahitaji mwalimu wa kipekee na myenye vipawa aweze kupitia kila kitu kingine kilichoongezwa katika miongo na karne.

 

Dini imekuwa palliative. Imekuwa distraction badala ya mwangaza. Imekuwa kitu ambacho watu [hutumia] kutoroka dunia ya kutafuta faraja badala ya maandalizi ya kushiriki duniani kwa njia kubwa.

 

Muumba anayajua haya yote, bila shaka. Ufunuo umo zaidi ya mjadala katika eneo la juu. Umo zaidi ya uvumi. Umo zaidi ya itikadi. Umo zaidi ya teolojia ya dini moja inayoshindana na teolojia ya dini ingine. Mashindano haya ni tatizo la binadamu lililoumbwa na kutokuelewana kwa binadamu na kikomo cha uwezo na kikomo cha hekima ya binadamu.

 

Unaweza kupinga hoja dhidi ya Ufunuo, lakini huu ndio Ufunuo ambao umetolewa, na utakuwa ni Ufunuo ambao umetolewa. Ukubaliwe au ukataliwe, huu ndio Ufunuo.

 

Mungu hashuguliki tu na dunia hii, lakini Mungu anajua kuwa dunia hii iko – mahali padogo katika ulimwengu mkubwa.

 

Uwepo wa Malaika unayosimamia dunia hii unatafsiri Nia ya Muumba katika maneno na matendo, Mafundisho na Ufafanuzi ambao watu wa dunia wanaweza kuelewa na kufanya leo na kesho na siku zijazo.

 

Munaulizwa mupokee, sio muhukumu.

 

Munaulizwa mujiandae kwa dunia, sio mtumie dini kama aina ya kutoroka dunia.

 

Munaulizwa muheshimu asili yenyu ya ndani na muchukue Hatua kwa Knowledge ndio ukweli wake uwe wazi kwenyu.

 

Munaulizwa muwache migogoro yenyu yasioisha na musifikiri kuwa munaweza kuwa na vita duniani kwa jina la Mungu, kwa kuwa hilo ni chukizo. Hakuna majeshi takatifu. Hakuna kitu takatifu kuhusu vita.

 

Munaulizwa mujifundishe na mujitayarishe kukabiliana na dunia mpya na kukabiliana na ukweli wa changamoto na fursa ya kuibuka katika eneo kubwa la waangavu ulimwenguni.

 

Hamuwezi kujifunza haya yote, kwa kuwa hamujui ya kutosha. Na kubishana na haya ni kuonyesha kikomo chenyu na kutoelewa kwenyu.

 

Ujumbe Mpya umeletwa kwa watu – sio wataalamu, sio viongozi, kwa kuwa wamewekeza mengi katika cheo chao na matokeo ya haya ni, hawawezu kuyaona yanayokuja au hawawezu kushiriki ukweli kwa wale wanawafuata.

 

Ufunuo unampa mtu binafsi nguvu kubwa sana, lakini pia wajibu mkubwa sana. Kama munaongozwa na nguvu ya Knowledge ndani yenyu, akili kubwa ile Mungu ameiweka ndani yenyu, basi hakuwezi kuwa na vurugu, vita na migogoro. Kutakuwa tu na juhudi ya kuanzisha mipango chanya ya faida kwa wengine.

 

Hii ndio kazi ya akili. Hii ndio changamoto kubwa kwenyu, changamoto cha kiasi kikubwa kuwa itachukua nishati yako yote kama unataka kuifanya kwa mafanikio.

 

Ufunuo umo zaidi ya eneo na fikio la akili. Umo zaidi ya eneo na fikio la imani na itikadi. Mungu haumbi itikadi. Mungu anawapa hekima na uwazi na kiwango cha juu cha kuishi. Munaweza tu kuamua kuyafuata ama kuyakana.

 

Amua kuyafuata, na muyafuate kwa rehema, bila kuyatumia kama silaha ya kudhulumu wengine au kulaani wengine. Kulaani wengine kwa kuzimu na hukumu ni kutoelewa Ufunuo wa Mungu wa sasa na wa kale.

 

Kutangaza kuwa hakuwezi kuwa na Ufunuo mpya ni kutangaza kiburi na ujinga wako na kufikiri kuwa unajua mengi kuliko Muumba. Kwa kuwa hakuna aliye duniani anayejua kile Mungu atafanya tena. Hata Uwepo wa Malaika haujui kile Mungu atakifanya tena, hivyo ni nani anayeweza kutangaza hivyo? Hakika huu ni mfano wa kiburi na ujinga!

 

Hakuna mtu duniani anayeweza kutangaza kuwa Jesu ndiye njia ya kipekee kwa Munngu kama Mungu ametoa njia zingine! Wewe ni nani wa kuyasema hivyo? Huku ni kutoelewa na kuchanganyikiwa. Hivyo ni kujaribu kuweka imani yako juu na zaidi ya imani za wengine, kufanya mwalimu wako, mwakilishi wako, kuwa mkubwa na wa kipekee wa kufuatwa. Haya sio mapenzi ya Mbinguni. Huu ni ujinga wa binadamu

 

Dunia ambayo itawakabili itahitaji ushirikiano mkubwa wa binadamu, huruma na mchango, ama itakuwa uwanja wa vita kuhusu nani atakuwa na rasilimali zilizobaki duniani. Nani ambaye anaweza kulinda mali yake wakati mataifa mengine yanashindwa na kuanguka?

 

Madai kwa binadamu yatakuwa makubwa mno kiasi cha itachukua huruma na hekima kubwa ili watu waweze kujibu. Lakini watu wamegawanyika sana. Dini zimegawanyika sana. Kikundi hiki kinapinga kikundi kile kwa jina la utawala wa taifa yao, au kwa mapenzi ya Mungu, na ubinadamu utatumbukia katika vurumai.

 

Hii ndio maana Ufunuo Mpya umo duniani. Hapa haumusifu Mtume kama Mungu. Unamuheshimu kama Mtume. Hapa hautangazi mawazo yako juu ya mwengine, lakini unatambua kwamba mawazo ni chombo tu cha kutumiwa na nguvu kubwa ndani yako na kwamba ukweli wa kweli, ukweli mkubwa, unaishi zaidi ya eneo la akili, akili ambayo kamwe haikuundwa kuelewa hali halisi zaidi ya maisha.

 

Mapenzi ya Mbinguni ni ubinadamu uungane na ujiandae ili uweze kuishi katika Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko na ujiandae kwa mahusiano yake na maisha katika ulimwengu kwa njia ambayo uhuru wa binadamu na uwezo wake wa kujitawala katika dunia hii unaweza kulindwa.

 

Kwa kuwa munakabiliwa na ulimwengu ambapo viumbe havifanani na binadamu kwa tabia au mawazo na ambapo uhuru ni nadra na ambapo mataifa na watu walio huru lazima zitumie busara kubwa na tahadhari kubwa kati ya uwepo wa mataifa mengi ambapo uhuru umezuliwa ama ambapo kamwe haujawahi kufahamika.

 

Mahitaji ya Jumuiya Kubwa yatakuwa makubwa. Hamuwezi kuwa mukihusika katika migogoro ya mara kwa mara hapa duniani na kuwa na uwezo wa kuishi kuwa dunia iliyo huru katika uwanja huu mkubwa wa maisha. Hili sio suala la mtazamo au imani. Ni jambo la lazima.

 

Ndiyo mataifa yaweze kuishi katika mazingira ya rasilimali zinazopunguka duniani na mageuzi ya kisiasa na kiuchumi na shida inayoongezeka, Itakuwa ni lazima mushirikiane na wengine kati yenyu. Badala ya vita, lazima mutafute njia za kutoa chakula cha kutosha, maji na nishati kwa watu wa dunia. Hiyo ndio haja ya kuhodhi itakayokuwa hapa duniani katika mustakabali.

 

Watu ambao wanafikiri venginevyo wanaishi kwa mtazamo wa siku zilizopita, Dhana zao zina msingi katika siku zilizopita. Hawawezi kuyaona yale yanayotokea kati yao. Hawawezi kuyajua yale yanayokuja katika upeo wa macho. Wanaishi katika shell yao ya imani na dhana zao na ni kama vipofu kwa ukweli wa dunia wa leo na kesho. Wanafikiri kuwa ushiriki wa ulimwengu utakuwa ni matokeo ya uchunguzi wa binadamu, lakini kesi hii ni nadra ulimwenguni. Maingilio hutokea wakati mataifa yanapata nguvu na yanaungana. Hapa ndipo changamoto ya uhuru na uwezo wa kujitawala wa mataifa huanza.

 

Mafundisho yenyu kuhusu ulimwengu na matayarisho ya kuishi katika dunia mpya ni makubwa sana, yanahitaji Ufunuo Mpya kutoka kwa Mungu. Uwazi wa asili, dhamira na umoja wa kiroho cha binadamu sasa lazima yasisitizwe zaidi ya mambo yote, ama binadamu hatapata nguvu ama umoja wa kujibu mabadiliko makubwa yalio juu yake.

 

Ufunuo Mpya unaleta usahihi na ufafanuzi mkubwa, ambao ni muhimu sasa kama dini zote za kitamaduni za dunia zitaongeza hekima kwa familia ya binadamu na sio tu kuongeza migogoro, ubaguzi na ugomvi. Kila mmoja ina mchango wa kufanya. Zote ni muhimu. Dini moja sio kuu zaidi kuliko ingine. Kufikiri hivi ni kutoelewa Mapenzi ya Mbinguni, kwa kuwa ni binadamu tu iliyo na umoja ambayo itakuwa na uwezo wa kushindana na changamoto za maisha katika dunia mpya na changamoto kubwa ya kuhifadhi uhuru wake na uwezo wa kujitawala mbele ya vikosi ulimwenguni.

 

Huu ndio wakati munaishi, katika wakati wa Ufunuo. Ni wakati muhimu. Ni wakati wa ugumu. Ni wakati wa machanganikio. Ni wakati wa matokeo makubwa.

 

Nyinyi ndio miongoni wa wakwanza kujibu Ufunuo Mpya. Na hii ni kwa sababu ya dhamira. Sio ajali kuwa hivi ndivyo ilivyo. Wewe ambaye bado unajaribu kupanga utimizo wako maishani bado haujagundua kuwa una dhamira kubwa hapa, dhamira itakayoelezwa kwa kipekee katika maisha yako, lakini ni dhamira unayoshiriki na wengine, kwa kuwa hakuna aliye duniani kwa ajali sasa.

 

Kila mtu alitumwa hapa kushindana na hali ya dunia. Lakini maandalizi hayo hutokea katika eneo la ndani zaidi ya akili, katika eneo la Knowledge. Hii ndio sehemu yako ambayo haijawahi kutenganishwa na Mungu. Ni sehemu yako ambayo ilikuwa, na bado, ni utambulisho wako wa kweli. Knowledge ndiyo ilikuleta duniani. Ni Knowledge ambayo itakuongoza ukichukua safari yako duniani. Itakuwa Knowledge ambayo itaibuka nawe nje ya dunia.

 

Waliojitenga wanakombolewa kupitia Knowledge. Waovu huokolewa kupitia Knowledge. Wajinga hufanywa wa hekima kupitia Knowledge. Hivi ndivyo Mungu huokoa, sio tu familia ya binadamu, lakini uumbaji wote ambao unaishi katika utenganisho, unayoishi katika ulimwengu wa kimwili ambao unaweza tu kufikiria.

 

Ni Mapenzi ya Mbinguni ujibu Ufunuo Mpya. Ni Mapenzi ya Mbinguni uchukue Hatua kwa Knowledge, kwa uvumilivu, bila dhana, ukiweka imani zako, mapendeleo yako na hofu zako kando ukiendelea ndio uweze kushiriki na nguvu kubwa, uadilifu mkubwa na dhamira kubwa ndani yako.

 

Ni Mapenzi ya Mbinguni kuwa muweze kushiriki uwazi na maandalizi haya kwa wengine na muwe

kama gari la kushiriki Ufunuo huu, kwa kupointi kwa Ufunuo Mpya.

 

Ni Mapenzi ya Mbinguni kwamba ubinadamu upevuke, uibuke kutoka ujana wake ulio reckless na wa utata kuwa mawakili wa hekima wa dunia hii, ulinde rasilimali zake za uzima za dunia hii na uwe taifa iliyo na huru katika ulimwengu ambapo uhuru ni nadra na huthamaniwa na wachache tu.

 

Ni Mapenzi ya Mbinguni muwache migogoro yenyu isiyoisha, kwa kuwa sasa hamuwezi kuharibu watu wenyu na miji yenyu . Mutahitaji rasilimali zote za dunia, rasilimali zote zile munazo, kushindana na Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko yanayokuja.

 

Hamuishi katika wakati wa siku zilizopita. Dunia ya kale imepita. Munaishi katika dunia mpya – dunia ya hali ya hewa isiyotabirika na mabadiliko ya hali ya mazingira, dunia ya rasilimali zinazopunguka, dunia ya udhaifu mkubwa, ya wasiwasi kubwa , ambapu tamaduni ya binadamu imo hatarini.

 

Lakini nani atayaona haya? Nani atayasikia haya, sio kwa dhana zake, au maoni yake au imani yake, lakini kwa undani, undani zaidi? Ni nani aliye na ujasiri wa kukabiliana na haya? Ni nani aliye na unyenyekevu wa kukabiliana na Ufunuo Mpya? Ni nani anayeweza kukubali kuwa Mungu ana mengi ya kusema kwa binadamu na awache ubinafsi, na kukemea na maazimio yanayofuata.

 

Mapenzi ya Mbinguni na nia ya binadamu bado ni tofauti sana. Lakini giza inaingia duniani, Hakuna wakati wa kutosha, na hakuna wakati wa upumbavu na kukana.

 

Ni wakati wa Ufunuo. Ni zawadi ya binadamu, ipokewe au ikanwe. Ni mustakabali wa binadamu, utimizwe au uharibiwe. Ni ahadi ya binadamu, igunduliwe na ielezwe au iharibiwe na itupwe. Huu ni uchaguzi mkubwa, sio wa watu wengine mahali pengine, lakini wako mwenyewe, ndani yako.

 

Kila kitu kinalingana na uchaguzi wa mtu binafsi, na hiyo ndio sababu Ujumbe Mpya kutoka kwa mungu unazungumza kuhusu swala hili. Hautoi tu mfumo mpya wa imani, nira mpya ya itikadi ambayo kila mtu sasa lazima aifuate na akandamizwe. Watu lazima watengeze maelezo kikamilifu. Lakini motisha lazima iwe ya kweli. Ufahamu lazima uwe hapo.

 

Lazima kuwe na uwazi mkubwa kuhusu yale munakabiliana nayo na yale mutakabiliana nayo katika mustakabali, na hii itarudisha nyuma tabia zenyu za udhaifu na uharibifu. Hii itafanya uwaze kabla ulaani ama ushambulie watu wengine au taifa zingine. Hii itarudisha nyuma extremesim na ukali na kiburi na ujinga wote unaojitokeza kwa uharara na ufasaha duniani.

 

Lazima uyasikilize maneno haya kwa roho yako. Usisubiri, kwa kuwa kila siku ni muhimu sasa. Wakati hauwezi kupotezwa sasa. Mtume yupo hapa. Hatakua hapa milele. Umebarikiwa kumusikia na kukutana naye kama inawezekana. Anabeba Ufunuo, zaidi ya kile ambacho kinapatikana katika kitabu au rekodi.

 

Mupokee, Musikilize. Na maisha yako itaonyesha ushahidi wa ukweli ambao unakaa naye na ndani yake na kupitia kwake.