Tag Archives: The Gift of a New Life

Zawadi ya Maisha Mpya

 

Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu hauko hapa tu kuongeza thamani kwa maisha yako ya sasa ama kuhalalisha mawazo na shughuli zako za sasa. Haiko hapa kuhalalisha dini za dunia ama kuendana na imani au matarajio yao, kwa kuwa Mungu hajafungwa na haya yote. Haiko hapa kuhalalisha matarajio yako, kwa kuwa Muumba wa Ulimwengu yote hajafungwa na haya.

Kwa kweli, Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu uko hapa kutoa maisha mapya kwa wale ambao wanaweza kujibu kwa kweli, kuwapatia msingi mkubwa ambapo wanaweza kujenga maisha ya maana – maisha ya kutia moyo, maisha inayoongozwa na Knowledge, maisha ya mahusiano ya kweli na ya ushiriki wa maana na dunia.

Hapa majukumu hayapewi, lakini watu wanapewa msingi ndio Knowledge ndani yao, Nguvu kubwa ile Mungu amewapatia iwaongoze, iweze kuwa wazi kwao, ndio waweze kwa wakati kujufunza kuiamini na kuifuata, wakipitia hali ngumu ya maisha na hali ngumu ile itabidi wakabiliane nayo katika dunia mpya ya rasilimali ambazo zinapunguka na hali kubwa ya ukosefu wa utulivu.

Watu wanakuja kwa Ujumbe Mpya kuona kama inaendana na imani yao, mawazo yao na matarajio yao. Bila Shaka, haifanyi hivyo.

Watu wanakuja kwa Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu wakitaka kuitumia kama rasilimali ya kupata kile wanachokitaka kwao wenyewe, lakini Ufunuo Mpya una mpango mkubwa na ahadi kubwa kwao.

Watu wanakuja kwa Ujumbe Mpya wakitarajia kuwa watapata hekima wanayohitaji kurekebisha makosa yao na kufanya uwekezaji wao uwe na mafanikio na maana, lakini Ujumbe Mpya uko hapa kuwapa maisha mapya – sio tu wazo mpya iliyowekwa juu ya maisha yao ya zamani, sio tu asali ya kufanya ladha ya uchungu ya maisha yao ya sasa iweze kuwa nzuri na kukubalika. Watu wana matarajio madogo na wanataka kidogo, na matarajio yao hayalingani na maana na nguvu ya Ufunuo.

Watu wanakuja kwa Ufunuo wa Mungu wakitaka kuona vile wanaweza kuitumia kwa sasa, kama Ufunuo tu ni mfululizo wa vyombo ambavyo watu wanaweza kutumia kuboresha maisha yao. Lakini hawawezi kuboresha maisha yao kwa sababu hawajui wanachofanya. Hawapajui wanapoenda, na mawazo yao na imani yao, kwa mara nyingi, hayalingani na dhamira yao kubwa na mwelekeo wao wa kweli maishani.

Watu wanaweza kufikiri kuwa Mungu ni mkubwa na haeleweki, lakini wanajaribu kutumia Mungu kama aina ya mtumishi, kijana wa kutuma ujumbe wa tamaa, matarajio na shida zao. Wanasema, „Basi, ni nini Mungu anaweza kufanya kwangu? Ufunuo Mpya wa Mungu unaweza kuniletea nini?“

Unaweza kuona kutokana na maswali haya kuwa mtazamo na matarajio yao sio halisi. Hakuna mnyenyekeo. Hakuna heshima. Hakuna uelewa kuwa wanajadiliana na kitu kikubwa mno kuliko uelewa wao, kinachozidi matarajio yao, maadili yao na mapendeleo yao. Kwa hivyo ni nini Mungu anaweza kuwafanyia ila kuwatia moyo kupitia mabadiliko na disappointents za maisha ili waweze kukuja kwa ushiriki huu mkubwa na nia safi na mwelekeo wa unyenyekevu?

Ujumbe Mpya uko hapa kuokoa binadamu kutoka kwa msiba na kutiishwa katika ulimwengu mukianza kuibuka ndani ya Jumuiya Kubwa ya waangavu, Jumuiya Kubwa ambayo mumekuwa mukiishi na ambapo sasa itabidi mujifunze kukabiliana nayo.

Lakini uko hapa kuwapa watu binafsi ufarisi mpya, msingi mpya na fursa ya kurejesha maisha yao, kujikomboa na kutumia uwezo wao na nguvu ya Knowledge ndani yao ili waweze kutumikia dunia ambayo mahitaji na shida yake yanaaza kuzidi kila siku.

Watu wengi wamekata moyo katika utafuti wa maana kubwa, ama bado hawajauzalisha kabisa. Kwao Ufunuo Mpya utakuwa wa udadisi au kitu cha kuhukumu., kitu ambacho wanakitolea hofu yao, hukumu yao na malalamuko yao bila hata kuelewa kile wanachokitazama.

Kutakuwa na aina mingi ya majibu kwa hii, bila shaka, lakini itakuwa muhimu kwa wale ambao wanajibu kwa nia nyenyekevu na aminifu na safi watambue kuwa nguvu na uwezo wa Ufunuo wa Mungu na kile Ufunuo unaoweza kufanya kwao – kuwarejesha kuwapa dhamira na mwelekeo mkubwa, ambao tayari unaishi ndani yao.

Huvumbui dhamira na mwelekeo, kwa kuwa tayari umo ndani yako, unaweza kuona. Ni sehemu ya blueprint ya asili yako ya ndani, zaidi ya eneo ya akili. Zaidi ya majadiliano na uvumi. Unaweza kujadiliana nayo milele na milele, lakini inamanisha tu kuwa haujaelewa.

Ni muhimu kuwa watu ambao wanakuja kwa Ufunuo kwa uaminifu, wawe na uelewa hapo awali kuwa wanakabiliana na kitu kikubwa mno. Sio mafundisho tu kati ya mengine. Sio ahadi tu ambayo itawapa kile wanachotaka maishani. Ni wa eneo tofauti kabisa. Ndio maana ni Ufunuo Mpya kutoka kwa Mungu, Ufunuo peke yake kutoka kwa Mungu duniani kwa sasa.

Hii haimaanishi kuwa Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu utajenga maisha mapya kwako na ikupatie juhudi ya kufanya, kwa kuwa hii lazima itoke ndani yako – kati yako wewe mwenyewe, kati yako na ushiriki wako na maisha.

Watu wengi watahitaji Ujumbe Mpya uwe msingi wa mazoezi na focus yao, na watu wengine wataitwa kutumikita Ujumbe Mpya kwa sababu ni wito wao. Lakini kwa wengine, utawapatia nguvu ya kutambua mwelekeo mkubwa na kuwapatia nguvu na uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi yalio muhimu na kupiga kona ambazo lazima zipitiwe ili wasonge katika mwelekeo chanya na wa maana.

Kuna watu wengi duniani leo ambao wanajua kuwa lazima wajitayarishe kufanya kitu, ambao wanahisi wito wa ushiriki mkubwa, ambao wanahisi kuwa maisha yao ni muhimu kuliko shughuli za kawaida za kila siku. Baadh yao hawatapata njia katika duni za kitamaduni za dunia kwa sababu wanatayarishwa na wanaitwa kufanya kitu duniani. Wana muungano mkubwa wa mustakabali kuliko siku zilizopita, na mustakabali unawaita na unawavuta waende mbele.

Kuna watu ambao wana hatima ya kupokea Ufunuo wa Mungu kuusoma na kufanya mazoezi yake. Hawatapata njia yao popote pengine. Kama una hatima ya kitu cha ukubwa huu, hutapata uridhika ama utimizo popote pengine – ukijaribu kiwezekanacho, ukiamini kikamilifu iwezekanavyo. Ukijaribu kubadilisha maisha yako kama dikteta, bado hutaweza kufanya ushiriki wa msingi ila maisha yako inaelekea katika mwelekeo sahihi na asili ya ushiriki ambao unafaa kuwa wako unaweza kutambuliwa kabisa na kukubaliwa.

Ni kwa watu hawa ambao Ufunuo utatoa maisha mapya, sio tu kufanya maisha yao ya zamani iwe bora, sio tu kuhalalisha yale ambao wameyafanya ama hawajafanya hapo awali. Sio to kuwatia moyo na kuwaambia, „Basi, uko sawa. Kile umakifanya ni sawa. Ni kizuri.“

Hapana, Ufunuo utafanya makosa yako yawe wazi,dissapointments zako ziwe wazi, uhisi ukosefu wa mwelekeo kwa kiasi kikubwa. Labda utafanya mateso yako yazidi hapo mwanzoni hadi uweze kutambua zawadi ya kweli ya Ufunuo na utambue kuwa unaanza safari kubwa sana, labda safari ambayo umefunga kwa muda fulani ambayo sasa inaaza kuenda haraka.

Hapa hakuna mahali pa maafikano. Huwezi kujadili na Mungu. Huwezi kujadili na dhamira na hatima yako, kwa kuwa huwezi kuyabadilisha. Unaweza kuyaepuka, kuyakana ama kupitia njia ya kuyakubali na kuyadai.

Jinsi dhamira yako itaelezwa itategemea na hali ya dunia intakavyobadilika. Kwa hivyo kila kitu hakikuamuliwa hapo awali, bila shaka. Mafanikio au kushindwa kwako hakutalingana tu na ushiriki wako, lakini pia kwa ushiriki na utayari wa wengina ambao wana hatima ya kuwa na jukumi kubwa katika maisha yako. Wakishindwa hapa, itaathiri matokeo kwako, kwa kuwa maendeleo yako yanategemea maendeleo ya watu wengine maalum.

Utekeleza huu wa azma sio wa mtu binafsi ambapo unajaribu kujierevusha mwenyewe. Ni kujiunganisha na uungano na wenginw kwa dhamira kubwa. Wakishindwa, itaathiri matokeo kwako. Ukishindwa itaathiri matokeo kwao. Hii ndio maana kushindwa hapa kuna matokeo makubwa. Unafikiri kama bado unaishi katika utenganisho, kwa hivyo huwezi kuona hatima yako imeunganishwa na wengine.

Hawa ndio wale wengine ambao ni lazima uwapate maishani. Labda utu wao hautakuwa wa haiba ama kuwa na nyuso nzuri na tabia neema za jamii ambazo huvutia watu wengi. Labda hawatakuwa watu ambao ungewapenda ama una ushirika nao katika wakati uliopita. Wengi wao hawatashiriki maisha yako ya mustakabali nawe hata kama ulikwa na ushiriki nao katika wakati uliopita. Utahitaji Knowledge sasa. Kwa kuwa hiyo peke yake ndani yako ndio itajua. Itaona. Na itajibu.

Kama mtu mwengine bado hayuko tayari, basi, itakuwa janga kubwa kwako. Hii haimaanishi kuwa maisha yako yameisha. Inamaanisha kuwa itabidi mpango mwengine utengenezwe kwako. Na matokeo ni safari yako itakuwa ndefu na haitakuwa ya uhakika.

Kuna mengi hapa ya kutupa. Kuna ushawishi mingi ambao hautoi matokeo na ambao unaharibu mtu binafsi. Kuna matarajio mengi ambayo yanakuongoza ujitolee kwa kitu kabla haujajua kile ambacho unakifanya maishani, kabla haujaunda uhusiano na Knowledge, ambayo peke yake inashikilia dhamira yako na hatima yako kubwa.

Daima Mungu hatafunua yoyote kwa akili yako, sehemu ya akili yako ambayo imeshawishiwa na dunia na haiwezi kutegemewa na ni dhaifu na inaweza kushawishiwa kwa urahisi na nguvu zengine. Hapana, zawadi inapewa kwa sehemu yako ya ndani ambayo haiwezi kushawishiwa na dunia, haiwezi kushawishiwa na hisia na tabia zako ambazo zinabadilika, matumaini yako, hofu yako, furaha yako, janga yako – haiwezi kushawishiwa na haya yote. Inaishi katika kina cha bahari, sio katika ubapa wa mtikisiko.

Kuchukua hatua kwa Knowledge basi kunakuwa ni muhimu, ama maisha yako itakuwa maisha tupu – ukikimbilia watu, ukikimbilia ahadi, ukikimbilia tamaa zako, ukikimbilia ndoto, ukikimbilia matumaini, ukikimbia hofu, ukiogopa kuwa labda umepotea na uko peke yako, ukiogopa kuwa maisha yako hayatawahi kuwa sawa.

Knowledge inaishi zaidi ya eneo la tamaa na hofu, na hii ndio maana kuwa ina utulivu. Hii ndio maana ina nguvu. Hii ndio maana haibadiliki, na hauwezi kuibadilisha. Hii, hata hivyo, inawakilisha ukombozi wako. Licha ya kile unafikiria ama unafanya ama umefanya ama hujafanya, nguvu ya ukombozi inaishi ndani yako.

Sio lazima Mungu achambue hali yako. Mungu wa ulimwengu hajishughulishi na maisha yako. Lakini Mungu ameweka Knowledge ndani yako, inabeba ahadi yako na mwelekeo wako. Itawapata wale watu unafaa kuwapata. Italeta masahihisho, maelewano na balance katika maisha yako kama utaweza kuitambua na kuifuata na kuitimiza, pale ambapo inahitajika.

Hii ndio inajenga maisha mapya – sio maisha ya zamani ambayo yamerekebishwa, sio maisha ya zamani na mfumo mpya wa imani, sio maisha ya zamani na seti mpya ya nguo ama ufafanuzi wa dini wa kuvutia ambao sasa umekubaliwa katika jamii kwa sababu unasema na unafanya yale yote yalio sahihi.

Wewe sio aina ya mtangazo wa imani ya mtu mwengine. Kuna ahadi kubwa yako. Mungu anajali maisha yako kwa sababu Mungu anakupatia maisha mapya. Vinginevyo, Mungu angewacha kila mtu ashindwe na hangeshughulika nao. Hii ndio watu kwa ukweli wanaamini kwa sababu ukifikiri Ufunuo zote za Mungu zilipewa karne iliyopita na Mungu hana chochote cha kusema kwa binadamu, basi lazima uhitimishe kuwa Mungu hajali binadamu na hana chochote cha kusema binadamu akikabiliwa na vizingiti sasa, zote, ambazo binadamu hajawahi kukabiliwa nazo.

Mutakabiliana aje na dunia ya upungufu? Mutakabiliana aje na maingilio kutoka mataifa ya unyama kutoka ulimwengu ambayo yako hapa kupata faida kutokana na udhaifu na utenganisho wa binadamu? Mutakabiliana aje na mageuzi ya kisiasa na kiuchumi cha kiwango ambacho hakijaonekana hapa duniani?

Kama wewe ni mwaminifu, lazima uone kuwa hata hauna kidokezo. Lakini hii ndio hali ya dunia na kile lazima wewe na wengine pia mukabiliane nayo.

Mungu ametuma maandalizi ya Dunia Mpya kama sehemu ya Ujumbe Mpya. Mungu anatuma mipango ya maandalizi ya kuanza kuimarisha maisha mapya. Kuna Ujumbe wa dunia na kila mtu ndani ya dunia. Tena kuna Ujumbe wa mtu binafsi ambye anahisi kuwa ana dhamira kubwa na hatima duniani. Lazima kuwa uamue kama hii inakuzungumzia.

Mungu hakuvumbua dhana na imani yako. Mungu hakuvumbua mapendeleo yako na hofu yako. Mungu hakuvumbua dunia ambayo ni bidhaa ya mapendeleo na hofu ya kila mtu. Huwezi kulaumu Mungu kwa sababu ya hali ya kijamii ya binadamu. Huwezi kulaumu Mungu kwa sababu ya vita na ukatili, unyonyaji, utumwa na umaskini. Haya yote ni uvumbuzi wa binadamu yalio na msingi katika uchoyo na ujinga, yalio na msingi katita uchangiaji wa watu wachache tu duniani.

Lakini Mungu alivumbua uwepo wa Knowledge ndani yako, na ni Ufunuo Mpya wa Mungu ambao unafanya hii iwe wazi, bila kufunikwa na historia ama utafsiri wa binadamu na kuchanganya uelewa wako. Mfulilizo uko wazi. Ujumbe ni safi. Unaupokea kutoka chanzo chake, badala ya utafsiri ambao ulitolewa karne iliyopita kwa matumizi ya binadamu.

Kuwa na maisha mapya, lazima ufanye kazi. Sio uchawi unaowekwa kwako. Sio kuchukua maji ya uchawi na kufanya kila kitu kiwe tofauti. Sio aina ya addiction ama intoxication.

Lazima ufanye kazi. Lazima uchukue hatari, Lazima ufanya maamuzi. Lazima ukose kutimiza matarajio ya watu wengne. Lazima ukose kutimiza matarajio ya malengo na tamaa yako. Lazima ubadilishe mipango yako.

Hapa ndipo unapata nguvu. Hapa ndipo unaungana na wewe mwenyewe. Hapa ndipo ushirika wako wa kweli unaibuka kati ya uazimaji na wajibu wako kwa wengine. Hapa ndipo unapata nguvu yako na unaweza kujiamini. Hapa ndipi unawacha kuwa na tabia ya ujinga, ukitoa maisha yako kwa mambo ya ujinga na yasio na maana. Hapa ndipo unajua wale wa kuchagua kuwa nawe na jinsi ya kuepuka majaribu ambayo yatakuongoza pengine.

Unapata nguvu kwa sababu Knowledge iko ndani yako. Unavumilia matatizo kwa sababu Knowledge iko ndani yako. Unaweza kukabiliana na uchungo na upotevu, ugonjwa na hata kukataliwa na wengine ambao wanakujali kwa sababu nguvu ya Knowledge iko ndani yako. Na ukikutana na mwengine ambao ameendesha nguvu hii, uhusiano wako utakuwa katika eneo ingine – ya ajabu duniani, ukiwa na uwezo wa kutengeneza vitu vikubwa kuliko vile wewe peke yako unaweza kutengeneza.

Mungu anakupatia chanzo cha nguvu, lakini lazima ufanye mazoezi ya uongozi wake, na lazima uendeshe ujuzi wa kibinafsi ambao unakuwezesha uwe chombo cha Knowledge – mtu wa nguvu na uadilifu, mtu ambaye anayeweza kusisimua wengine na anaweza kuleta uwezo wa kujiamini, faraja na mwelekeo kwa wengine.

Huu ndio Ufunuo Mpya wa Mungu. Hii ndio inafaa kuzalisha. Lazima kuwe na wachagiaji walio na nguvu duniani sasa, ama binadamu atakabiliwa na upungufu mkubwa mno.

Uwache huu uwe uelewa wako.