Miadi Takatifu

Una hatima ya kukutana na watu fulani katika maishani. Una miadi nao. Wataongozwa kukutana na wewe kama vile unaongozwa kukutana nao. Mahusiano hayana msingi kutoka ufarisi wa maisha zilizopita duniani, lakini ni sehemu ya mpango ulianzishwa kabla uje diniani, mpango ambao uliundwa kukuwezesha utambue dhamira kubwa katika maisha yako. Mungu anajua huwezi kutambua na kutekeleza dhamira hii peke yake, kwa sababu ni maalum na tofauti kuliko kitu chochote duniani. Itapinga ufafanuzi na ulinganisho, kwa kuwa inaongozwa na Nguvu Kubwa na Hekima Kubwa zaidi.

Lakini huwezi kupata dhamira hii peke yako. Unaweza tu kuandaa njia kwa dhamira hii. Unaweza tu kuandaa akili yako na hali yako ili dhamira hii kubwa zaidi ijitokeze. Na ikinaanza kujitokeza, itabadilisha jinsi unajiona na unaona ulimwengu wako.

Mahusiano ni njia, lakini pia ni thawabu. Kwa sababu hakuna kitu kinachoweza kufanywa peke yake duniani. Hata kama unafanya kazi peke yako na unaishi peke yako katika upweke, chochote unachoweza kuunda bado ni mchakato wake na wengine. Ni mchakato wa kuunganisha akili yako na akili zengine- katika kesi hii, akili ambazo ziko zaidi ya eneo inayoonekana – kutoa kitu cha maana na muhimu mkubwa.

Hii ndio mwanamichezo anataka kwa kufikia nguvu zaidi na uwezo. Hii ndio mwanamuziki anataka kwa kuruhusu mchakato wa ubunifu ujitokeze. Hii ndio kila mtu anataka kwa kutafuta maana katika dunia, utafutishi ambao unaweza tu kutimilizwa na dhamira kubwa, iliyowatuma hapa mwanzoni.

Huwezi kufanya hata maandalizi ya dhamira hii kubwa peke yako, kwa utahitaji wengine ambao wanaweza kukusaidia na kutambua thamani yake ndani yako. Haya ni mahusiano ya kipekee. Hazijaimarishwa ndio uweze kupata fursa. Hazijaimarishwa kutimiza matarajio yako au ndoto zako. Zina jukumu kubwa zaidi, jukumu ambalo ni muhimu uipate nguvu ya kuheshimu kile kilicho ndani zaidi unachokijua. Inatoa mahusiano ya muda mfupi na inayodumu.

Hapa mahusiano ya muda mfupi ni kama alama, inayopointi njia, kukumbusha kwamba una wajibu mkubwa katika maisha. Hapa watu wataingia maisha yako kwa muda mfupi kusisimsha Knowledge ndani yako, au kutoa choto muhimu ya hekima ambayo unahitaji ili uweze kuendelea. Unaweza kuwa na mahusiano mengi kama haya kwa muda fulani, na kila moja utakusaidia kutambua njia yako na kupata nguvu ya kusafiri katika mwelekeo ule, ambao ni tofauti na ule kila mtu anaufuata.

Alafu utakuwa na mahusiano ambayo ni ya muda mrefu, hasa ukiendelea na kupata ufafanuzi zaidi na nguvu, na ukiweza kupata uhuru kutoka ahadi zako za awali na wajibu na ukiweza kutambua ndoto zako na hali ya mahusiano yako.

Hapa unaanza kufikia pointi ya maidi na wale ambao watachukua nafasi muhimu zaidi katika maisha yako, lakini hata kama muna hatima pamoja haimaanishi mutapatana. Kwa sababu kuna vitu vingi vinazoweza kukuwalisha nyuma. Kuna hatari nyingi zinazoweza kuzuia musiweze kufika katika pointi ya miadi. Kuna maamzi mengi ambayo yanaweza kugeuza maisha yako iende upande tofauti.

Kwa hivyo unaweza kufika pointi ya miadi na upate wengine hawajafika. Waliitolea maisha yao huko nyuma, na hata kwa wengine, walipoteza maisha yao. Na hii ni shida kubwa mno, unaweza kuona, kwa sababu wanamiliki sehemu ya misioni, misioni ambayo pia ni yako. Na kama watu wa kutosha hawatafika, misioni yako itakuwa hatarini.

Hapa kile unachoweza tu ni kuifanya sehemu yako peke yake kikamilifu iwezekanavyo na uombe kwamba wale ambao una hatima ya kukutana nao – ama pia wale bado hawako tayari – wafuate nguvu ya Knowledge iliyo ndani yao, akili ya ndani ile Mungu ameweka ndani yao iwaongoze, iwalinde na iwalete katika miadi hii takatifu.

Watu hufikiri dhamira yao ni kitu ambacho wanaweza kujitengenezea, ile wanafikiri itawafurahisha na ile wanaamini itawapa utimizo. Lakini bila Knowledge kama kiongozi na mshauri wako, mipimo hii haitakuwa sahihi na kwa mara nyingi itasababisha maisha yako ielekee mwelekeo tofauti, mbali na pale unahitaji kuenda na mbali na miadi takatifu ile unafaa kuwa nayo na wale wako hapa kushiriki dhamira kubwa zaidi na wewe.

Mara mingi watu huoa ama huolewa na kutolea maisha yao kabla wajue ni nini wanafanya, kabla ya kuwa na hali halisi kuwa wana mwelekeo na njia kubwa ya kufuata. Na miadi yao ikikaribia, wanatukutika, wanakuwa na wasiwasi na wanachugachuga, wakihisi kuwa kuna mahali wanahitaji kuwa ambapo ni tofauti na pale walipo.

Kama haufuati njia yako halisi maishani, daima utakuwa na wasiwasi, na wasiwasi hii na kutokuwa na uhakika itarudia mara kwa mara kwa sababu moyoni wako unajua huendi mahali unahitajika, hufanyi kile unahitajika kukifanya, na maisha yako haisongi mahali inapaswa kusonga. Hapa hakuna kiasi cha furaha au vikwazo au tiba inaweza kufuta usumbufu huu, kwa sababu ni ishara kuwa maisha yako ina hatima na ni lazima uifuate hatima hii. Ahadi yako kwa hii lazima iwe kuu zaidi kuliko mapenzi au fedha. Ni lazima iwe kubwa kuliko tamaa ya mali na usalama, hata mafanikio kama vile dunia inafasili mafanikio.

Kila mtu anaitwa, lakini ni wachache tu wanajibu. Usipojibu, hatimaye utapotea duniani, na tajiri au maskini maisha yako itakuwa ya kukata tamaa- itakuwa ya kushindwa, na kuchanganikiwa itakayokuwa ya kudumu.

Ukikosa ishara nyingi, ukitia shaka kile kinachoanza kujitokeza kutoka ndani yako, hatimaye utahisi kuwa umepotea, na hata mali yako itakuwa kama janga kwako. Kile ambacho kilitakiwa kununua furaha, ridhaa na uhuru hakitaweza kukutolea chochote hapa.

Zaidi ya mahitaji ya mwili na mahitaji ya akili, kuna mahitaji ya roho. Mahitaji ya roho yanaweza tu kutimilizwa ukihitimiza dhamira kuu yako na kuhitimiza miadi yako na wale ambao wanashiriki dhamira hii na wewe na watachukua nafasi katika ugunduzi wake na uelezo wake.

Hakuna hakika kila mtu atafika. Na ni miujiza kwa wale watafika kwa sababu ilibidi wafuate kile ambacho hakiwezi kuelezwa ili wapate njia ya kufika huko. Ilibidi wawezane na shuku zao za kibinafsi na mashawishi ya wengine ili waweze kufika katika miadi hii takatifu. Ilibidi waamini kile ambacho labda hakuna mwengine katika maisha yao aliamini ama kudhamini. Ilibidi wajitolee kwa uadilifu wao na hisia ambazo ziliwashawishi ni nini ambayo ni sahihi kwao.

Dunia daima hujaribu kukushawishi ukitake kile ambacho, au ukihitaji kile ambacho na uwe yule ambaye hawakilishi asili yako ya ndani zaidi. Ushawishi huu wa kupotosha huathiri kila mtu kwa digrii mbalimbali. Hata watu waasi dhidi ya maadili ya utamaduni bado huathiriwa na maadili haya. Kwa hivyo kuwa mwaasi peke yake haitoshi, kwa kuwa mpaka wakati ule utagundua mwelekeo mkuu zaidi na sauti iliyo ndani yako, bado utadhibitiwa na hali ya kijamii yako, iwe uikumbatie ama uikatae. Hakuna uhuru hapa.

Hapa unaingia jangwani. Unaondoka ile njia nzuri ile kile mtu anasafiri, na unafuata njia tofauti na ile haiwezi kufafanuliwa katika maisha yako. Hii ndio njia ambayo walii wote na wachangiaji kwa binadamu walisafiri, na ilibidi wasafiri bila idhini ya familia na marafiki wao. Ilibidi wasafiri bila idhini ya dunia. Ilibidi wasafiri bila uadui, bila kulaani wengine na bila kukana dunia kwa jumla. Kwa sababu ni dunia hii ulikuja kutumikia katika siku zijazo na ukiikana, hautakuwa katika nafasi ya kuitumikia kwa dhati.

Miadi ndiyo kila mtu anatafuta bila kufahamu kwa tamaa yao ya ushiriki, mapenzi na mahusiano. Hapa haja za akili, na haja nyingi za akili kwa kweli sio halisi, yanashindana na yanavurugia haja ya ndani ya nafsi. Watu hawatambui kuwa haja yenyewe ni ya kweli na ni halisi. Katika eneo ya ndani kabisa, ni msingi wa mafanikio na dhamani ya maisha yako na matimizo.

Lakini watu hawana uvumilivu. Wanataka mashirikiano sasa. Wanataka kutimiza ngono sasa. Wanataka kutimiza matarajio ya utamaduni kwa kuwa na familia sasa. Hawana nia ya kungoja. Wanaogopa wakingoja, miadi haitatokea. Kwa hivyo watu wanachukua hatua mapema. Wanaoa au wanaolewa kabla kuwa tayari. Wanapata watoto kama bado hawako tayari. Wanatolea maisha yao kwa kazi bila kuwa tayari. Ule muda wanakuwa nao katika mwanzo wa maisha yao kuchunguza na kufarisi mwelekeo wa ndani katika maisha yao mara nyingi hupotea kwa shughuli nyingine, hutumiwa kufuata tamaa zingine ama hukatwa kabisa kawa sababu ya madai na matarajio ya wengine, na kwa ukosefu wa uvumilivu wao wenyewe.

Hapa watu ambao wana mchango mkubwa wa kufanya duniani huishi maisha isiowakilisha asili yao halisi. Na kwa hakika, mahalalisho yamo kila mahali. Lakini watu wakiishi maisha ambayo haiwakilishi asili yao halisi na dhamira yao, daima wataishi maisha ya uchugachuga. Na wakikosa kuanza safari ya Hatua kwa Knowledge, tabia yao itakuwa ya upotofu na uharibifu wa kibinafsi kesi ikithiri. Na washirika wao hawataelewa tabia hiyo au asili a kutoridhika kwao.

Kwa hivyo watu hukabiliana na hii kwa kutimia hobbies zao, michezo na tabia obsessive. Ama wanameza madawa ya kulevya au kunywa pombe, wakijaribu kuzuia hisia inayojitokeza kwa muda kuwa hawako pale wanahitajika na hawafanyi kile wanafaa kukifanya. Kuwa wana ahadi zengine tofauti na kuna wale wanategemea watimize ahadi hizo. Kwa hivyo mgogoro wa ndani unakua. Kama watu wakianza safari yao kwa kutafuta mwelekeo wa ndani katika maisha yao, makosa haya yatakuwa adimu na ngumu kufanya.

Kwa hivyo watu hukosa miadi yao. Na hata kama wamefanikiwa katika maisha na wamepata maadili ya utamaduni, watahisi upungufu. Watahisi hali ya kushindwa, na hali ya majuto. Huwezi kubadilisha hii kwa njia ya mazungumzo, au kwa njia ya tiba au kwa njia ya kile utakachojiambia kwa sababu asili yako ya ndani ni asili yako ya ndani. Na kwa sababu una dhamira kubwa maishani iliyo asili na ya kipekee kwako, huwezi badilisha hali hii. Mwelekeo wa ndani unaojitokeza ni kitu ambacho huwezi kukana bila kuzalisha migogoro na vivinyovinyo ndani yako.

Na haitoshi kumuamini Mungu na kumuabudu Mungu, kwa kuwa kama huwezi kufuata kile Mungu amekiweka ndani yako kukifuata, kama huwezi kufuata Knowledge iliyo ndani yako ile Mungu ameiweka ikuongoze, basi maombi yako na kusujudu wako kwa kweli sio halisi. Unaweza muomba Mungu akupe neema, unaweza muomba Mungu akuokoe kutoka shida kubwa na ndogo, lakini haukuweza kufika pointi ya miadi na Mungu. Pointi ya miadi na Mungu ni pointi ya miadi na Knowledge ndani yako, kwa kuwa hapo ndipo Mungu huwasiliana na wewe. Hapo ndipo unaungana na Chanzo cha maisha yako.

Hapa kuna shida hata kama wewe ni mtu wa dini. Hapa dini inaweza kuficha uchugachuga na ukosefu wa utimilifu. Imani katika mafundisho ya kidini, kanuni za dini au imani ya kidini inaweza kuficha na kubadilisha jukumi ya msingi ile wewe unayo ya kujibu nguvu na uwepo wa Knowledge ndani yako. Ukikosa kujibu nguvu na uwepo huu, utakuwa mtumwa wa nguvu zengine, na hisia yako ya uhuru na hisia ya ustawi na utimilifu wako utakuwa dhaifu na utatoweka.

Hatimaye hili ni swala la utenganisho. Wale ambao wanaamini utenganisho ni ya ukweli na wanaweza kujitimiza kupitia mawazo yao na imani yao na tamma zao, hawatambui kwamba wana uhusiano wa msingi na Mungu, Muumba wa maisha yote. Unaweza kubishana daima na uhusiano huu na hisia ya dhamira, lakini huwezi kuitokomeza. Itakufuapa popote utakapoenda. Daima hutaweza kuitikisa kwa sababu hauwezi kujitenganisha na Mungu. Hauwezi kujitenganisha na maisha.

Kwa hivyo kusudi yako ikizidi, ukizidi kujaribu kuyakidhi mahitaji yako ya ndani kupitia matendo ya nje na ukizidi kujitolea kwa shughuli zako, kwa hobbies zako na matarajio yako, utazidi kujiimarisha dhidi ya miadi hii ya kimsingi ambayo unayo na Knowledge ndani yako.

Hapa huwezi kufanya mpango. Huwezi kujadiliana na Mungu na kusema, “Naam, mimi nitakupa sehemu kidogo ya maisha yangu kwa kile unachotaka, kama naweza kupata ninachotaka.” Hapa hakuna majadiliano. huwezi kujadiliana na Muumba wa Ulimwengu. Huwezi kujadiliana na nguvu ya Knolwedge ndani yako. Watu wale wanaofikiria hivyo hufikiri Mungu na Knowledge ni rasilimali zinazoweza kutumika kutimiza mahitaji ya kibinafsi, zinazoitwa zikitajikana, zinazotumiwa zikitajikana, vile unavyoweza kuita idara ya polisi au idara ya moto ukiwa na tatizo.

Hilo ni kosa kubwa tena sana. Na matokeo yake ni ya kutisha kwa sababu watu hudhamini kilicho kidogo au kile hakina thamani na wanakosa kile kilicho na thamani kubwa sana. Wanachagua kuimarisha imani zao na wale ambao watathibitisha imano hao. Hivyo hata hapa mahusiano yao yanafanya kazi dhidi yao.

Huwezi kutengua ukweli kwamba ulitumwa hapa kutimiliza dhamira kubwa. Unaweza kufikiri hii ni ukiukaji wa uhuru wako, lakini uhuru ni zawadi uliopewa ili uweze kugundua kile kilicho cha kweli na muhimu ndani yako, na uweze kufanya ugunduzi huu peke yako bila ugunduzi huu ulazimishwe kwako na nguvu kubwa ya kigeni. Watu wale huamini utenganisho hawapendi hii. Wanafikiri inakiuka uhuru yao. Wanafikiri ni aina ya udikteta wa Mungu katika ulimwengu. Wao huona ni kama kulazimishwa na sio kama zawadi ya ukombozi kama vile ilivyo.

Kwa hivyo kuna tatizo za msingi katika uelewa wa watu. Lakini hatimaye swala ni, unaweza kufika pointi ya miadi na Knowledge na pia na wale walio hapa kushirikiana nawe katika dhamira kubwa inayojitokeza katika maisha yako? Hii ndiyo utatafakari wakati utatoka katika maisha hii na kurudi kwa familia yako ya kiroho, kikundi chako cha masomo. Hawatashugulika na hobbies zako ama yale uliyoshugulika nayo. Hawatashigulika na majanga yako au makosa yako, mapenzi yale uliyoyapoteza ama shuguli zako za kiuchumi ulizoshindwa nazo. Hawatashugulika na tabia zako zisio za kawaida ama tabia za kipekee za maisha yako iliyopita. Watashugulika tu na kama ulifika pointi ya miada na Knowledge na wale ambao walitumwa kukutana nawe. Watakuangalia na watauliza, “Ulifanikiwa?” Na hautaweza kuwafichia ukweli, kwa kuwa zaidi ya dunia ni vigumu sana kudanganya katika mahusiano.

Hii ndiyo itakuwa muhimu mwishoni. Mambo mengi yalio muhimu kwako sasa ama yale unayokabiliana nayo sasa hayatakuwa muhimi mwishoni. Watauliza, “Ulifika pointi ya miadi? Ulifanya kile ulichotumwa kukifanya?” Na itabidi uwaambie ukweli kwa sababu itakuwa wazi kwa wote. Na kutoka kwa mtazamo huu utaweza kuona waziwazi, bila kikwazo.

Kwa hivo ni nini kiingne unaweza kukifanya ili kurudi na kujaribu tena. Hakuna “siku ya hukumu”, pale ukishindwa katika maisha moja utaenda jehanamu ya milele. Huu ni uvumbuzi wa binadamu. Lakini matokeo ya kutopata dhamira yako na kujaribu kuishi bila dhamira hii ni ya kweli na ni dhahiri kila siku katika mawazo yako, na mwenendo wako, tabia yako na ufarisi wako. Bila dhamira hii unaishi katika aina ya jehanamu – jehanamu iliyo nzuri, lakini jehanamu ambayo huwezi kuwa na furaha, ambapo daima hauwezi kuwa katika hali ya raha kwa sababu hauheshimu asili yako ya ndani.

Knowledge iko haka kuelekeza maisha yako katika mwelekeo fulani, lakini kama haufuati mwelekeo huo, ama haujaenda katika mwelwkeo huo utakuwa katika hali ya uchugachuga. Lakini uchugachuga huu haufai kukanwa ama kuepushwa. Ni wito wa utambuzi na azimio. Hii ndio maana Mungu hahukumu. Mungu huvutia na kuajiri. Dhana nzima ya jehanamu ni jinsi binadamu anajaribu kuwaadhibu wale hawezi kuwakubali, na kutimia Mungu kama mwaadhibu. Ni ya kulipiza kisasi. Ni chombo cha akili kuwaadhibu akili zengine, au kuzilazimusha ziamini, kuzilazimisha kwa nguvu ziamini kukubaliana na makubaliano.

Una miadi takatifu na Knowledge kupitia seti ya makutano yatayobadilisha mwendo wa maisha yako na kukufunulia asili yako ya ndani na ukweli wa ndani unaozidi mawazo yako yale yanayokuhusu, utu wako na historia yako ya kibinafsi – utambuzi ulio zaidi ya eneo na ukfikia wa akili.

Alafu una miadi na watu wengine. Miadi zingine zitadumu muda kidogo, na wale watakuja maisha yako kwa muda mfupi kukukumbusha kitu fulani, kukufundisha kitu fulani ama kusemea kitu ndani yako inayohitaji nishati na upya.

Alafu una miadi na wale watachukua nafasi kubwa katika maisha yako, wale wako hapa kutumikia kwa kiasi kikubwa kile ambacho hao wenyewe wanaanza kukitambua ndani yao. Wale watakaofika katika pointi ya miadi watachukua nafasi kubwa katika maisha yako na watasimama kinyume na mahusiano yeyote uliojaribu kuanzisha.

Kama utaweza kukutana na watu hao, utaona utofauti katika maisha yako, na utagundua kwamba kile ambacho umekua ukikifuata ni cha ukweli na hautafunga safari hii peke yako. Ukipanda mlima huu – hasa ukifika sehemu za mwinuko – utahitaji mahusiani makuu. Pengine moja wa watu hawa atakuwa bwana ama bibi yako. Pengine atakuwa mtu ambaye munagawana kazi yenyu kubwa zaidi pamoja. Pengine itakuwa mwalimu aliye hapa kukutia moyo uendelee na ushinde ukiendelea. Inawezekana kuwa moja wa watoto wako, anayetambua asili yako kubwa na yule maisha yake imeunganishwa na wewe kwa kueleza kitu cha kipekee na muhimu duniani.

Mahusiano yanaweza kuchukua fomu tofauti. Lakini ukifika katika pointi ya miadi, itakuwa wazi kuwa mahusiano yako kwa kweli inahusu kitu kiingine, zaidi ya vigezo vya mahusiano ya binadamu vya kawaida. Zitasemea kile kilicho ndani na kilicho kikubwa. Ni ya ajabu. Ina maudhui zaidi na takatifu. Ni kitu ambacho kiko zaidi ya eneo ya akili, kwa hivyo kinakosa ufafanuzi. Maneno yako na majaribio yako kuyaeleza yanaweza tu kukaribia maana kamili. Haya ni mahusiano takatifu, ni takatifu kwa sababu ya nia yao na asili yao ya ndani.

Miadi hii yakitokea katika kiasi hichi, hakutakuwa na uhakika wa mafanikio kwa sababu lazima mupambane na hali yenyu ya jamii, asili yenyu ya dunia na shida zote ambazo hujitokeza katika kujiimarisha na kujidumisha maishani. Miadi sio hatua la mwisho, bali ni chanzo na uanzishaji wa hatua ya pili katika maisha yako.

Hapa mzigo ule ulikuwa ukiubeba kwa muda mrefu unaanza kupata maelezo katika maisha yako na hasa katika mahusiano haya, na utaanza kushukuru na kuhisi muinuko. Utauhisi upya na uhakikisho kuwa kwa kweli unafuata kitu muhimu, kuwa haujidanganyi na kwa kweli zina nguvu kubwa na ukweli mkubwa kwa maisha yako. Mahusiano haya yatatoa ushahidi wa jambo hili. Yatashuhudia jambo hili. Siri itakuwa nawe na kati yenyu – siri ambayo hamutaweza kufafanua, lakini ambayo lazima mujifunze kuitegemea na kuithamini juu ya vitu vyote.

Uhusiano wako na Mungu daima hautaweza kuelezeka. Hauwezi kuufunga ndani ya seti za imani, kanuni au mafundisho. Kufanya hivyo ni kuiweka ndani ya kaburi. Daima iko hai na inabadilika. Daima itakuangazia maisha yako na kukuongoza ufuate mambo fulani na kukupeleka mbali na mambo mengine, kama beacon kubwa inayokuongoza nyumbani – kutoka utenganisho, kutoka jehanamu ya utenganisho wako, kutoka migogoro yako ya zamani isiyo na suluhisho, kutoka tabia za madhara zile unashinda ukizirudia, kutoka ndoto zako, kutoka mishwasha, kutoka hatia, kutoka kushindwa.

Ni jambo la kushangaza kwamba wale ambao watajibu na kufika katika pointi ya miadi takatifu ni watu ambao wameshindwa kujitimiza duniani. Na labda watafikiri kuwa ni watu ambao wameshindwa duniani. Wameshindwa kupata mapenzi ama mali ya kutosha. Ama wameyapata haya, na kugundua kuwa hayatimizi mahitaji yao. Kwa hivyo kuna hisia ya kushindwa na disillusionment. Lakini kushindwa huku na disillusionment ni muhimu. Wakati kila mtu anajaribu kuepuka kushindwa na disillusionment, haya mawili yanatayarisha watu kugundua ukweli wa ndani unaoishi ndani yao.

Kama umeshindwa kufika katika pointi ya miadi, baadaye katika maisha, ukigundia maneno haya, kuna ukombozi wa pili. Na hii ni kuchangia kwa wengine – kuchangia mali yako, kuchangia wakati wako na kuchangia chochole unachoweza kuchangia katika huduma ya mahitaji halisi ya watu na dunia karibu na wewe. Huu ndio ukombozi wa pili. Hauna nguvu na utimizo kama wa kwanza lakini ni muhimu na utakuwa na ufanisi. Wale ambao wamekuwa na nia isiyoeleweka watapata mwishoni ya maisha yao kuwa wana fursa ya kuchangia, kuwa wafadhili – wafadhili wa mali, kama wana mali; wafadhili wa wakati, wakiwa na wakati; wafadhili wa huduma, wakiwa na nguvu ya kutoa huduma. Kwa hivyo kuna ukombozi wa pili.

Lakini kilicho muhimu kwa watu wadogo na wale walio katika umri ya kati, ni kuzingatia miadi takatifu – kuomba wafanikiwe, kuuliza wafanikiwe, kuambia Ulimwengu, “Chochote kitachohitajika kufanywa ili niweze kufika katika pointi hii ya miadi, lazima nifike pointi hii. Lazima niijue dhamira kubwa inayoishi ndani yangu.”

Ukiwa ambivalent kuihusu, ukiiogopa, ukiwa katika migogoro kuihusu, hautafika katika pointi hii ya miadi. Kwa hivyo lazima ukichague utakachokithamini. Na kama umepata hekima ya kutosha maishani – kupitia mafanikio na kushindwa, kupitia majalio na nuhusi – utajua jinsi ya kuchagua kisahihi. Utaona kuwa dunia inaweza kutoa furaha na huzuni, lakini sio utimizo.Hii lazima itoke kutoka sehemu ingine, kutoka Ukweli Mkubwa unaoishi ndani yako, ndani ya Knowledge.

Kuna sababu unatafuta katika mahusiano, lakini sio uridhike, upate mali ama kwa sababu ya tamaa. Kuna sababu zaidi. Na ingawa utashindwa mara mingi katika mahusiano, kamwe hautakata tamaa kwa sababu unatafuta miadi takatifu yanayokusibiri na yalio muhimu katika utimizo na mafanikio katika maisha yako.