Kufahamu Mungu

Sasa ni wakati wa ufahamu zaidi wa Mungu na kupanua uelewa wa Mungu. Mungu ndiye chanzo cha na mwandishi wa maisha yako na maisha ya wote duniani na katika Jumuiya Kuu ya mataifa yote ambayo wewe huishi. Uelewa huu mpya sio wa kukosoa uelewa wa awali, ila ni wa kuupanua, kuukamilisha zaidi na kuuwacha mlango wazi kwa ufarisi wa mapenzi ya Mungu hudhurio ya Mungu katika maisha yake.

Kwa kuwasilisha Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu, ni muhimu basi kufufua ufarisi huu wa Mungu- kuufufua, ili kuutenganisha na yale yote am-bayo taasisi za binadamu na uvumbuzi ule binadamu alioongeza, na kuuleta katika lengo kubwa zaidi na na kwa uwazi kwako.

Hapa ni muhimu kutochanganya Mungu na dini, kwa sababu mambo mengi ya kutisha yalifanywa kwa jina la dini na kwa jina la Mungu. Lakini Mungu huishi mbali zaidi ya mambo yote haya, mbali zaidi ya makosa ya binadamu,mbali zaidi ya mawazo ya binadamu, mbali zaidi ya uvumbuzi wa binadamu na mbali zaidi ya ufisadi wa binadamu.

Sasa ni muhimu kwako wewe kufikiria Mungu ndani ya uwanja mkubwa wa waangavu ambao wewe unaishi, ambao umo pamoja na maisha yote duniani na unaelekea zaidi ya dunia hii, ndani ya Jumuiya kuu ya Mataifa yote.

Kuwa na uzoefu safi wa ukeli wa Mungu na mapenzi ya Mungu kwa maisha yako, lazima upate ufahamu huu mkubwa, kutoka kwa Jumuiya Kubwa, wa Mungu. Ila, unaweza kufikiria Mungu kama makadirio ya maisha yako mwenyewe na asili ya mwanadamu, kama makadirio ya hisia yako mwenyewe, mawazo na maono yako. Utasihia kwa Mungu hasira yako, mapendekezo yako, hukumu yako, mapendekezo yako ya kulipa kisasi, mawazo yako ya haki na adhabu na kadhalika.

Hata hivyo, Mungu huishi zaidi ya haya yote. Mungu wa ukweli, Mungu wa usafi ambaye amekuwa anang`aa kama jua juu yako. Bila kujali mawingu angani, bila kujali uchafuzi wa mazingira katika anga na bila kujali masumbuko katika ardhi. Mungu ni kama jua inayong`aa juu yako. Lakini Mungu huishi zaidi ya jua, zaidi ya ufafanuzi wowote unayoweza kufikiria, Zaidi ya historia yako, zaidi ya walimu wakubwa na watumwe wakubwa kutoka kwa Mungu, zaidi ya vitabu vikubwa vya kiroho na ushahidi, kuna Mungu, Muumba na mwandhishi wa maisha yako.

Kile Mungu alichokiunda kinaishi ndani yako. Kinaishi zaidi ya akili yako, zaidi ya fikira yako na ufahamu wako, zaidi ya dhana yako, zaidi ya mawazo yako na imani. Inaishi ndani yako, katika akili yako ya ndani, na Ujumbe Mpya unakiita Knowledge. Akili hii ya ndani ndiyo akili inayojua. Ni akili inayongojea.

Ni akili ambayo huona wazi bila kuvuruga, bila hofu, bila upendeleo, bila fujo na bila uvumi. Ni akili inayoishi ndani yako. Hii ndiyo Mungu aliyeumba ndani yako ambayo itadumu, ambayo itadumu milele.Zaidi ya utambulisho wa muda wako katika dunia hii, zaidi ya matukio yote ya dunia hii na zaidi ya uzoefu wako katika maisha haya, kuna Knowledge ndani yenyu, na Mungu ndiye mwandishi wa Knowledge hii.

Ukimfikiria Mungu katika muktadha huu mkubwa, unaweza kuanza kufahamu nguvu na ukuu wa uumbaji wa Mungu ndani ya ulimwengu na hata ndani yako mwenyewe. Mwili wako, akili yako na utu wako ni magari ya muda ambayo lengo lao ni kueleza uhusiano wako na Mungu na hekima ambayo Mungu amekupatia ili uweze kuwasiliana na kuchangia katika dunia wakati wa haja.Fikiria basi kama mwili wako, akili yako ni magari ya kueleza, na zina thamani,lakini sio muhimu kama kile ambacho zinafaa kueleza na kutumikia.

Basi utaanza kuona kwamba Mungu anaruhushu vitu vyote, Mungu anaishi ndani ya kila kitu, na bado Mungu ni zaidi ya kila kitu. Unaweza kuhisi uwepo wa Mungu popote ulipo, na unaweza kupata na kufuata Maarifa popote ulipo.

Kwa hiyo, kuelewa na kuhisi Mungu ndani ya maisha yako, lazima ukuje kwa Knowledge ndani yako, ambayo ni akili zaidi, ile ambayo itayodumu, ambayo Mungu ameumba ndani yako na kwa ajili yako. Knowledge ni asili yako ya ukweli. Zaidi ya mawazo yote, fikira na ndoto, ni asili yako ya kweli. Ni kwa kupata uhusiano na Knowledge, kwa kujifunza kupambanua Knowledge kutoka kito chochote na kufuata Knowledge ndio utaweza kujufunza na kutambua ufarisi wake, nguvu yake na mapenzi ya Mungu katika maisha yako.

Hata hivyo ujumla wa Mungu utakuwa milele zaidi ya dhana ya akili, zaidi ya uvumbuzi wote wa binadamu na zaidi ya filosofia zote za mtu binafsi na za watu wote. Ni seti gani za mawazo na dhana zinazoweza kufafanua Mungu wa Jumuiya Kubwa, Mungu ambaye ni mwandishi wa mataifa ya viumbe visiyoweza kuhesabiwa katika ulimwengu, mataifaa ya kipekee na tofauti na nyengine kwa njia nyingi?

Kukuja kwa Mungu basi ni kukuja kwa Knowledge ndani yako, kwa sababu Knowledge ndiyo itakayokuita kwa Mungu. Labda utaitwa kuenda mahali fulani au kwa mtu fulani, lakini ni kwa kusudi hii- kwa ufarisi wa uwepo wa Mungu ndani yako. Kwa sababu utahitaji zaidi ya imani kufahamu, kuelewa na kufuata kile ambacho Mungu amewapa kuona, kujua na kufanya.

Wacha basi hii iwe chanzo chako, ambapo utachukua hatua kwa Knowledge, ambapo utachukua hatua kwa Mungu. Ufanye hivyo hata kama wewe ni Mkristo, Buddhist, Muislamu au unafuata imani yeyote unayozingatia. Hata kama hauna imani, bado kuna hatua kwa Knowledge. Mungu ndiye alieumba dini zote duniani, na Knowledge ndiyo ambayo inayounganisha dini zote, licha ya matengano na vita zilizopo kati yao. Kwa kuwa matengano na vita ni uvumbuzi wa binadamu sio uzushi wa Mungu.

Wito unaduta ndani ya mila hizi zote-ndani yao na hata zaidi yao. Ni wito unaopatikana katike ulimwengu, unaoviita vyumba yva Mungu virudi kwa nguvu na hadhara ya Knowledge, kugundua kile Knowledge alichowapangia, kuona na kujua. Hii inaanzisha kurudi kwa Mungu– wito, kusikiliza, kukabiliana na kurudi.

Wacha basi huu uwe uelea wako